Israel yafanya mashambulizi katika ukanda wa Gaza kujibu shambulizi la maroketi
2021-05-11 08:37:40| CRI

Israel imefanya mashambulizi kwenye ukanda wa Gaza na kuwaua karibu watu 20 wakati maroketi yakiendelea kurushwa kutoka kwenye ukanda huo kuilenga Israel hadi jana jumatatu.

Baada ya mamia ya wapalestina kujeruhiwa kwenye mapambano na polisi wa Israel yaliyotokea jana katika eneo la Jerusalem mashariki, kundi la Hamas lilifanya shambulizi la maroketi dhidi ya mji wa Jerusalem na kufanya Israel ajibu vikali.

Wizara ya afya ya Gaza imesema watu 20 wameuawa ikiwa ni pamoja na watoto 9, na wengine 65 wamejeruhiwa kwenye milipuko iliyotokea katika mji wa Beit Hanoun, kaskazini mwa ukanda wa Gaza.

Hadi kufikia jana maroketi 100 yalirushwa kutoka Gaza na kusababisha majeruhi kwa watu wawili kwa upande wa Israel, maroketi mengi yalizuiwa kwa mfumo wa ulinzi wa anga wa Iron dome.