Israel yatangaza hali ya hatari katika mji wa katikati wa Lod
2021-05-12 16:40:01| cri

Ofisi ya waziri mkuu wa Israel imetoa taarifa kuwa, mji wa Lod ambao ni makazi ya Waarabu na Wayahudi umeingia kwenye hali ya dharura.

Taarifa hiyo imesema, waziri mkuu Bw. Benjamin Netanyahu amesema, ni lazima kupambana vikali na wahalifu, na kutumia zaidi jeshi la ardhini ili kurejesha utulivu na utaratibu wa mji.

Habari zinasema, mapambano kati ya Palestina na Israel yameendelea kutokea tangu kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Waarabu wanaoishi nchini Israel wamefanya maandamano kuunga mkono Wapalestina na kusababisha kuongezeka kwa vurugu kati ya jamii hizo mbili.