China yahimiza kuchukuliwa kwa hatua halisi kusaidia nchi zinazoendelea kupata chanjo ya COVID-19
2021-05-12 09:15:27| CRI

 

 

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Hua Chunying amesema, chanjo ni silaha muhimu ya kushinda janga la COVID-19, na badala ya kuwa na maneno matupu, jambo muhimu zaidi ni kuzisaidia nchi zinazoendelea kupata chanjo hiyo.

Muungano wa Chanjo Duniani GAVI umesema unawasiliana na kampuni kadhaa za China ili kupanua vyanzo vya chanjo vya mpango wa kimataifa wa kuratibu chanjo ya COVID-19, COVAX. Wakati huohuo, Marekani imetaka kusitisha ulinzi wa hakimiliki za chanjo ya COVID-19, huku ikiwa na wasiwasi kwamba teknolojia zake za matibabu zitachukuliwa na nchi nyingine.

Hua amesema hadi sasa China imetoa msaada wa chanjo ya COVID-19 kwa zaidi ya nchi 80 zinazoendelea, na kuuza chanjo hiyo kwa zaidi ya nchi 50. Licha ya hayo, China imetoa teknolojia za kutengeneza chanjo hiyo kwa nchi nyingine, na kushirikiana kimataifa katika uzalishaji wa chanjo hiyo. Amesema China inakaribisha nchi zenye uwezo kutoa chanjo kwa nchi zinazoendelea, ili kushinda janga la COVID-19 mapema na kwa pamoja.