Katibu mkuu wa UM aeleza wasiwasi wake kutokana na kupamba moto kwa mgogoro kati ya Palestina na Israel
2021-05-12 09:35:00| cri

 

 

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana alitoa taarifa kupitia msemaji wake akifuatilia kupamba moto kwa mgogoro kati ya Palestina na Israel.

      Taarifa hiyo imesema, vikosi vya usalama vya Israel lazima vijizuie kadiri viwezavyo, na kuepusha matumizi ya nguvu kupita kiasi. Amesema kitendo cha kurusha makombora na roketi kwenye maeneo ya wakazi ya Israel hakikubaliki. Na vitendo vinavyozidisha mgogoro lazima visitishwe. Umoja wa Mataifa unashirikiana na pande mbalimbali husika, ili kutuliza hali ya eneo hilo mapema iwezekanavyo.