Baraza la usalama la UM laitisha tena mkutano wa dharura kuhusu suala la Palestina
2021-05-13 09:35:20| CRI

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa jana liliitisha mkutano mwingine wa dharura kuhusu suala la Palestina, ambao ni wa pili ndani ya wiki hii. Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun ambaye ni mwenyekiti wa zamu wa baraza la usalama aliongoza mkutano huo na kufafanua msimamo wa China.

Bw. Zhang Jun amesema hivi karibuni hali ya ardhi iliyokaliwa ya Palestina inazidi kuzorota, vurugu na mvutano kwenye Jerusalem mashariki vinazidi kupamba moto, na mapambano makali kwenye ukanda wa Gaza yanaendelea na kusababisha vifo na majeruhi kwa raia wengi.

Amesema China inafuatilia kwa karibu hali ya Palestina na kulaani vikali vitendo vya utumiaji mabavu dhidi ya raia, na kuzihimiza pande husika hasa Israel zijizuie. na pia China inautaka Umoja wa Mataifa ufanye juhudi zaidi kutuliza mvutano kwenye kanda hiyo.