Waislamu wa Xinjiang washerehekea sikukuu ya Eid al-Fitr
2021-05-13 19:40:24| Cri

Waislamu katika mkoa unaojiendesha wa Xinjiang nchini China leo wamesherehekea sikukuu ya Eid al-Fitr, ambayo inaashiria kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadan.

Baada ya swala ya asubuhi, waislam kutoka makabila mbalimbali walisherehekea kwa kucheza dansi katika maeneo kadhaa ikiwemo uwanja ulio mbele ya Msikiti wa Id Kah, ulioko Kashgar.