China yaendelea kuchunguza anga ya juu kwa moyo wa kunufaisha binadamu wote
2021-05-17 19:23:52| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian, leo amesema China itaendelea kuchunguza anga ya juu kwa moyo wa kunufaisha binadamu wote, kuhimiza ushirikiano wa kimataifa kwa msimamo wazi, na kutoa mchango mkubwa zaidi wa kuchunguza anga ya juu na kuhimiza maendeleo ya amani ya binadamu.

Chombo cha anga ya juu cha China “Tianwen-1” kilitua kwenye sayari ya Mars tarehe 15. Mashirika na wataalamu wa nchi mbalimbali wameipongeza China kwa mafanikio hayo.

Bw. Zhao amesem, kama alivyosema rais Xi Jinping wa China kwenye barua yake ya pongezi, kutua kwa Chombo cha “Tianwen-1” kwenye sayari ya Mars ni hatua muhimu kwa China kuchunguza anga ya juu, na kutimiza safari kwenye sayari baada ya mwezi, kuweka alama kwenye Mars ni maendeleo muhimu ya mambo ya safari za anga ya juu ya China.

Bw. Zhao amesema anga ya juu ina ndoto ya pamoja ya binadamu. China siku zote inashikilia kutumia anga ya juu kwa amani, kufanya maingiliano na ushirikiano husika, na kunufaisha matokeo ya maendeleo ya safari ya anga ya juu.