Safari ya treni kati ya China na Ulaya zafikia elfu 38 kwa ujumla
2021-05-18 19:41:30| CRI

Safari ya treni kati ya China na Ulaya zafikia elfu 38 kwa ujumla_fororder_VCG111325558750

Msemaji wa ofisi ya utafiti wa sera katika kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Jin Xiandong leo amesema, katika miaka mitano iliyopita, safari za treni kati ya China na Ulaya zimefikia elfu 38 kwa ujumla, na kwenda katika miji 151 ya nchi 22 za Ulaya.

Amesema treni kati ya China na Ulaya zimesaidia nchi zilizoko kwenye kanda hiyo kuwasiliana na kuungana, kuzidisha ushirikiano wa kibiashara na maendeleo ya kuunganisha viwanda, kuinua hali ya kujulikana na sifa yake, na nchi na sehemu zinazopitiwa na treni hiyo zinashirikiana kwa wingi zaidi.

Takwimu zinaonyesha kuwa mwezi Aprili mwaka huu, treni 1,218 zimesafirisha makantena laki 1.17, ambalo ni ongezeko la asilimia 24 na asilimia 33 kuliko mwaka jana wakati kama huu.