Marais wa China na Serbia wafanya mazungumzo mjini Belgrade
2024-05-09 08:58:23| CRI

Rais Xi Jinping wa China jana Mei 8 alifanya mazungumzo na mwenzake wa Serbia Aleksandar Vučić mjini Belgrade, ambapo wakuu hao wa nchi hizo mbili wametangaza kuimarisha na kuinua uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote, na kujenga Jumuiya yenye Hatma ya Pamoja kati ya China na Serbia katika zama mpya.

Kwenye mazungumzo yao, Rais Xi amesema Serbia ni mwenzi wa kwanza wa kimkakati wa pande zote wa China katika eneo la Ulaya Mashariki na Kati. Ushirikiano kati ya nchi hizo mbili umetia msukumo mkubwa kwenye maendeleo ya kila upande, na kuleta manufaa halisi kwa wananchi wao. Amesisitiza hadhi muhimu ya kimkakati kati ya nchi hizo mbili, na kutarajia kuwa zitaelekeza vyema mwelekeo wa jumla wa uhusiano kati yao. Pia ametaka nchi hizo mbili ziendeleze ushirikiano halisi ili kunufaisha zaidi wananchi wake. Mbali na hayo, Rais Xi ametarajia nchi hizo mbili zipanue wigo wa ushirikiano na kuufanya ushirikiano wa ubunifu uwe nyanja mpya ya ongezeko kwenye uhusiano wa pande mbili.

Rais Vučić amesema, Rais Xi Jinping ni kiongozi mkubwa wa dunia, chini ya uongozi wa Rais Xi, China imepata mafanikio yasiyo kifani, imekuwa mnara wa maendeleo unaong’ara duniani, na imechukua nafasi muhimu ya uongozi kwenye mambo ya kimataifa. Amesema, kuinua uhusiano kati ya Serbia na China hadi kufikia ngazi ya Uhusiano wa Wenzi wa Kimkakati wa Pande Zote, na kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya Serbia na China, hakika kutakuwa mnara mpya katika historia ya uhusiano wa nchi hizo mbili. Serbia inaunga mkono kithabiti na itashiriki kwenye mapendekezo yaliyotolewa na Rais Xi, likiwemo Pendekezo la Maendeleo Duniani (GDI), Pendekezo la Usalama Duniani (GSI), na Pendekezo la Ustaarabu Duniani (GCI). Rais Vučić amesema, Serbia itaimarisha uratibu wa kimkakati na China, kupambana kwa pamoja na umwamba, kulinda Katiba na Kanuni za Umoja wa Mataifa, na kutetea haki ya kimataifa.