Umoja wa Ulaya wasitisha kuongeza hatua za kujibu kitendo cha Marekani cha kutoza ushuru kwa bidhaa za chuma na alumini
2021-05-18 09:01:57| CRI

Makamu mwenyekiti mtendaji wa kamisheni ya Ulaya Valdis Dombrovskis amesema Umoja wa Ulaya utasitisha kuongeza zaidi hatua za kulipiza kisasi dhidi ya Marekani kufuatia nchi hiyo kutoza ushuru kwa bidhaa za chuma cha pua na alumini, ili kutoa nafasi za mazungumzo kwa pande hizo mbili kujadili namna ya kutatua mgogoro kati yao.