Umoja wa Mataifa wajitahidi kuwahimiza Palestina na Israel kusimamisha mapambano.
2021-05-18 17:39:23| cri

Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stéphane Dujarric amesema, Umoja huo unajitahidi kufanya uratibu kuwahimiza kundi la wapiganaji la eneo la Gaza na Israel kusimamisha mapambano yanayoendelea kupamba moto kati yao.

Bw. Dujarric amesema Umoja huo unaendelea kuongeza uratibu kati ya pande husika. Katibu mkuu wa Umoja huo pia amezihimiza pande husika kusimamisha mapambano mara moja.

Bw. Dujarric pia amesema Umoja huo umepokea ripoti nyingi za wapalestina kupoteza makazi. Hivi sasa watu zaidi ya elfu 28 wamepoteza makazi, na wameomba msaada kwa Umoja huo.