Putin: Russia iko tayari kushirikiana na nchi zote kwa msingi wa kuaminiana
2021-05-19 08:50:54| CRI

Rais Vladimir Putin wa Russia amesema nchi yake iko tayari kushirikiana na nchi yoyote na kuanzisha ushirikiano wa kunufaishana.

Rais Putin amesema hayo kwenye hafla ya kupokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi wa nchi 23 iliyofanyika jana. Amesema Russia inapenda kushirikiana na nchi yote kwa msingi wa usawa, kuheshimiana na kutoingilia katika mambo ya ndani ya upande mwingine.