Naibu waziri mkuu wa China ahutubia mkutano wa kilele wa uwekezaji wa nchi za Afrika
2021-05-19 18:44:30| CRI

 

 

Naibu waziri mkuu wa China Bw. Han Zheng ameshiriki na kuhutubia mkutano wa kilele wa uwekezaji wa nchi za Afrika kwa njia ya mtandao, akihimiza ushirikiano wa kimataifa ili kuzisaidia nchi za Afrika kufufua uchumi.

Bw. Han amesema kutokana na janga la COVID-19, hivi sasa kufufuka na kuendelea kwa mwelekeo wa maendeleo ya nchi za Afrika ni muhimu sana, hivyo China imetoa mapendekezo manne kwa jumuiya ya kimataifa. Kwanza ni kutimiza ahadi ya kuisaidia Afrika kupunguza mzigo wa madeni. China inatekeleza pendekezo la kuchelewesha malipo ya madeni ya nchi za Afrika la kundi la nchi 20, na kupenda kuendelea kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kuzisaidia nchi za Afrika kupunguza mzigo wa madeni. Pili ni kufanya ushirikiano wa kunufaishana, ili kuhimiza kufufuka kwa uchumi wa Afrika. Pia amesema China inaunga mkono mashirika ya fedha ya kimataifa  na kampuni binafsi kuongeza uwekezaji katika nchi za Afrika, ili kuhimiza maendeleo endelevu barani Afrika. Tatu ni kuhimiza maendeleo ya uchumi kwa njia isiyoleta uchafuzi wa mazingira barani Afrika. Na nne ni kuhimiza mgawanyo wa haki wa chanjo ya COVID-19 kwa Afrika.