Mkuu wa masuala ya kisiasa wa UM aitaka jamii ya kimataifa kusaidia kupunguza mapigano kati ya Gaza na Israel
2021-05-19 09:09:03| CRI

Msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya siasa na ujenzi wa Amani, Bi. Rosemary DiCarlo amesema, jamii ya kimataifa inapaswa kufanya kila linalowezekana kupunguza mapigano huko Gaza na Israel, ambayo yamesababisha mamia ya watu kupoteza maisha na kupata majeruhi.

Bi. DiCarlo amesema hayo katika Jukwaa la Umoja wa Mataifa kuhusu Palestina, na kuongeza kuwa, mpaka sasa, Umoja huo umejihusisha kikamilifu katika upatanishi, na kwamba mapigano yanayotokea sasa kati ya kundi la Hamas na jeshi la Israel yanakumbusha haja ya kutafuta suluhisho la kumaliza kabisa mapigano kati ya Wapalestina na Waisrael.

Amesema kama mapigano hayo yataendelea, mahitaji ya kibinadamu yataongezeka zaidi, hususan katika Ukanda wa Gaza, ambako hali ya kibinadamu tayari ilikuwa mbaya.