China yaitaka Marekani iunge mkono Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kupunguza hali ya wasiwasi kati ya Palestina na Israel
2021-05-19 19:26:53| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian, leo amesema China inatumai Marekani itafuata ahadi yake, kurudi kwenye hali ya kuwepo kwa pande nyingi, kubeba wajibu wake wa nchi kubwa, kuunga mkono Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupunguza hali ya wasiwasi kati ya Palestina na Israel, kujenga upya hali ya kuaminiana na kutatua suala hilo kwa njia ya kisiasa.

Bw. Zhao amesema hivi karibuni waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ametoa pendekezo kuhusu kupunguza hali ya wasiwasi kati ya Palestina na Israel, ambalo limepongezwa na nchi za kiarabu na nchi za kiislamu. Nchi hizo zinaona msimamo na pendekezo la China limeonyesha wajibu wa China wa kuwa nchi kubwa na msimamo wa haki katika suala la Palestina.