China na Russia kuongeza kiwango chao cha matumizi ya nishati ya nyukilia kutokana na ushirikiano
2021-05-20 17:38:51| CRI

 

 

Marais wa China na Russia jana walishuhudia uzinduzi wa miradi ya ushirikiano ya nishati ya nyukilia, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vituo vya uzalishaji wa umeme kwa nishati ya nyukilia vya Tianwan na Xudabao. Wataalam wanaona kufanya ushirikiano katika matumizi ya nishati ya nyukilia kutasaidia nchi hizo mbili kuongeza uwezo wa teknolojia katika sekta hii.

Ushirikiano kwenye teknolojia ya nishati ya nyukilia umepewa kipaumbele katika ushirikiano wa jadi kati ya China na Russia, na umeendelea kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni. Mwezi Mei mwaka 2018, pande hizo mbili zilisaini makubaliano mbalimbali ya ushirikiano katika sekta ya nyukilia, na kuamua kujenga kwa pamoja vituo vya kuzalisha umeme kwa nishati ya nyukilia vya Tianwan na Xudabao. Mtafiti mkuu wa Tovuti ya Nishati ya China Bw. Han Xiaoping, amesema China na Russia zote zina teknolojia nyingi katika ujenzi wa vituo vya kuzalisha umeme kwa nishati ya nyukilia, na ushirikiano kati yao utanufaisha pande hizo zote, na kuzisaidia kuongeza zaidi kiwango cha teknolojia hizo. Anasema, “Nchi hizo mbili zote zina teknolojia nyingi. Russia ilianza kujenga vituo vya uzalishaji umeme kwa nishati ya nyukilia mapema sana. Kupitia ushirikiano huo, tutaweza kuendeleza teknolojia zetu. Hivi karibuni China ilianza kutumia kizazi cha tatu cha kinu cha nyukilia. Ushirikiano huo pia utazisaidia nchi hizo mbili kuweza kutumia zaidi nishati safi.”

Bw. Han amesema katika ushirikiano wa safari hii, nchi hizo mbili zimetumia kizazi cha tatu cha teknolojia ya nyukilia yenye usalama zaidi, na hali hii itasaidia pande hizo mbili kukuza ushirikiano wao kwa kina na mapana. Anasema, “Kizazi cha tatu cha teknolojia ya nyukilia ina usalama na ufanisi zaidi. Tuna njia kadhaa za teknolojia hiyo, huku Russia pia ina njia yake maalumu. Teknolojia hizo tofauti zimeunganishwa vizuri, zitaleta usalama na ufanisi zaidi. Licha ya hayo, Russia ina maliasili nyingi, na inaweza kuiletea China fueli ya nyukilia kwa ajili ya vituo vya kuzalisha umeme vya China.