Umoja wa Ulaya wapendekeza kulegeza vizuizi dhidi ya baadhi ya watalii waliopata chanjo
2021-05-21 19:34:48| cri

Baraza la Umoja wa Ulaya limependekeza nchi wanachama wake kulegeza vizuizi dhidi ya watalii wa nchi za nje waliopata chanjo kikamilifu.

Baraza hilo limesema nchi wanachama wa umoja huo zinaweza kukubali watalii wa nje waliokamilisha kupigwa chanjo zinazothibitishwa na idara ya usimamizi ya dawa ya Ulaya kwa siku 14, kutokuwa na haja ya kujitenga au kupima tena. Pia zinaweza kulegeza masharti ya watalii waliopata chanjo zilizothibitishwa na Shirika la Afya Duniani.

Baraza hilo pia limependekeza kulegeza vizuizi dhidi ya watalii kutoka nchi zenye chini ya maambukizi 75 mapya kati ya watu laki 1 katika siku 14 zilizopita.