Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Senegal wafanya mazungumzo kwenye simu
2021-05-21 09:16:46| CRI

Mjumbe wa taifa wa China ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi alifanya mazungumzo na mwenzake wa Senegal Bibi Aïssata Tall Sall kwenye simu.

Kwenye mazungumzo yao Bw. Wang Yi alisema kuwa, China na Senegal ni marafiki muhimu wa ushirikiano na pia ni nchi mwenyekiti za pamoja za baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika. Chini ya uongozi wa marais wa nchi hizo mbili, ushirikiano kati ya pande hizo mbili ulitekelezwa kwa kiwango kikubwa na kupata mafanikio makubwa. China itafanya juhudi pamoja na Senegal kukabiliana na changamoto ya janga la COVID-19, kuisaidia Senegal kuharakisha mchakato wa viwanda, kuongeza uwezo wa kujiendeleza, na kuendelea kuisaidia Senegal kupambana na janga hilo.

Bibi Aissata aliishukuru China kwa kutoa uungaji mkono katika kupambana na janga la COVID-19 kwa Bara la Afrika na Senegal. Amesema Senegal inaunga mkono na kupenda kushirikiana na China kutekeleza pendekezo la kuisaidia Afrika na kuendeleza urafiki kati ya China na Afrika.