Umoja wa Mataifa waihimiza Sudan Kusini kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu
2021-05-24 20:13:43| cri

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini imelaani mauaji ya kikatili dhidi ya mfanyakazi mmoja wa misaada ya kibinadamu katika kaunti ya Panyijiar na kuihimiza serikali kuhakikisha usalama wa wafanyakazi hao.

Mratibu wa masuala yakibinadamu wa UM nchini Sudan Kusini Bw. Alain Noudehou amesema, mashambulizi dhidi ya raia na mali za misaada ya kibinadamu yamevunja sheria za kimataifa za kibinadamu.

Bw. Noudehou pia amelaani shambulizi dhidi ya msafara wa wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu likiwemo gari moja la wagonjwa, ambalo limetokea kilomita chache na lilipotokea shambulizi lililoripitwa siku hiyohiyo huko Kocha. Kwenye shambulizi la kwanza daktari mmoja wa Kamati ya Uokoaji ya Kimataifa IRC aliuawa katika kituo cha afya cha Ganyliel Payam.