Changamoto ya taizo la ombaomba kwa serikali za miji na jamii
2021-05-25 16:33:05| Cri

Katika miezi ya hivi karibuni jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limekamata watu watatu eneo la Himo Wilaya ya Moshi kwa madai ya kujifanya wana ulemavu na kuomba msaada katika maeneo mbalimbali. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Amon Kakwale alisema kina Mama wawili huwa wanakaa mahali wanaomba watu wanawahudumia wakijua ni walemavu wanahitaji msaada, lakini ni watu wenye viungo vyote na wanaweza kutembea na kujipatia riziki kwa njia halali, lakini yupo pia kijana mmoja anayewapitisha maeneo mbalimbali akiwasaidia kuomba. Kamanda Kakwale ametoa wito kwa wananchi wanaojishughulisha na biashara ya kuomba wakijifanya ni watu wenye ulemavu, kuacha mara moja.

 

Tatizo kama hili pia limekuwepo hapa China kwa muda mrefu, lakini sasa kwenye maeneo ya mijini ombaomba hawaonekani tena. Ufanisi wa kuondokana na tatizo hili, unataokana na matumizi ya njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na udhibiti na hata kuwa na programu mbalimbali, kama vile kuwajengenea nyumba na hata kuwa na njia za kuwasaidia kiuchumi.