Katibu mkuu wa UM atoa pole kwa familia ya Yuan Longping
2021-05-25 09:25:04| CRI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UM) Bw. Antonio Guterres ametoa pole kwa familia ya mwanasayansi maarufu wa mpunga wa chotara wa China Yuan Longping, aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita, akiwa na umri wa miaka 91.

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema, Bw. Guterres na maofisa wengine wa UM wametoa salamu za pole kwa familia ya Bw. Yuan Longping, akisema wanaheshimu kazi kubwa ya Mwanaakademia Yuan alizofanya katika maisha yake yote, ambazo zimesaidia mabilioni ya watu kuboresha usalama wao wa chakula. "

Bw. Yuan aliyekuwa mwanachama wa Akademia ya Uhandisi ya China alikuwa ametafiti mpunga wa chotara kwa zaidi ya miongo mitano, na ameisaidia China kufanya mwujiza wa kufanikiwa kuwalisha karibu theluthi moja ya watu duniani kwa chini ya asilimia 9 ya ardhi ya kilimo duniani.