Serikali ya Japan yasema tahadhari ya usafiri iliyotolewa na Marekani haitaathiri michezo ya Olimpiki ya Tokyo
2021-05-26 08:51:45| CRI

 

 

Serikali ya Japan imesema tahadhari ya usafiri iliyotolewa na Marekani haitaathiri maandalizi ya michezo ya Olimpiki na kusafiri kwa ujumbe wa Marekani.

Kauli hiyo imetolewa baada ya Wizara ya mambo ya nje ya Marekani kuweka “tahadhari ya hali ya juu” kwenda Japan ikisema Japan kuna ongezeko la maambukizi ya COVID-19, kutokana na kuwepo kwa aina ya virusi vinavyoweza kuhatarisha hata watu waliopewa chanjo.

Katibu wa baraza la mawaziri wa Japan Bw. Katsunobu Kato amesema wanaamini kuwa hakuna mabadiliko ya msimamo wa Marekani kwenye uungaji mkono kwa serikali ya Japan kufanikisha michezo ya Olimpiki.

Waziri wa mambo ya nje wa Japan Bw Toshimitsu Motegi pia amesema tahadhari hiyo ya Marekani haizuii kabisa watu kusafiri kama kuna ulazima.