WHO: Hali ya ukosefu wa usawa katika ugawaji wa chanjo ya COVID-19 duniani yaongezeka
2021-05-26 08:46:06| CRI

 

 

Mshauri mwandamizi wa mtendaji mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Bw. Bruce Aylward, amesema hali ya ukosefu wa usawa katika ugawaji wa chanjo ya COVID-19 duniani inaongezeka.

Bw. Aylward amesema kati ya dozi bilioni 1.6 ya chanjo hiyo zilizotolewa, asilimia 83 zimetumiwa na nchi zenye mapato ya juu na ya kati. Licha ya hayo idadi ya upimaji wa virusi vya Corona unaofanywa kila siku katika nchi zilizoendelea, ni mara 125 kuliko ile ya nchi zinazoendelea. Amesisitiza kuwa kama virusi haviwezi kugunduliwa, maambukizi yake hayatazuilika, na hali hii italeta maafa makubwa.

Bw. Aylward amesema hivi sasa nchi maskini zinahitaji mitungi milioni 3.3 ya oksijeni, lakini zinaweza kupata kiasi kidogo tu.