China yasema tukio la Floyd lilionesha sehemu ndogo tu ya suala la ubaguzi wa rangi la Marekani
2021-05-27 16:14:07| cri

 

 

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian jana kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema, tukio la George Floyd lilionesha sehemu ndogo tu ya suala la ubaguzi wa rangi la Marekani, na Marekani inapaswa kushughulikia masuala yanayoikabili nchi hiyo, na kurudisha usalama kwa wananchi wake.

Bw. Zhao amesema, kutokana na takwimu zilizotolewa na tovuti ya Axios ya Marekani, katika mwaka mmoja uliopita baada ya tukio la George Floyd, uhusiano kati ya wamarekani wenye asili ya Afrika na polisi si kama tu haukuboreshwa, bali pia umegeuka kuwa msukosuko unaozidi kuwa mbaya siku hadi siku. Asilimia 72 ya wahojiwa wenye asili ya Afrika wanaona kuwa, vitendo vya polisi kuwapiga risasi vijana wa kiafrika vimekithiri nchini Marekani katika mwaka mmoja uliopita.