SOKA: Villarreal waifunga Man United kupitia penalt na kushinda taji
2021-05-27 17:10:14| cri

Miamba wa La Liga Villarreal ndio washindi wa Europa League msimu huu kwa magoli 11-10 kupitia mikwaju ya penalti dhidi ya Manchester United mjini Gdansk, Poland, katika mechi iliyochezwa jana usiku. Timu zote zilitoka sare ya 1-1 baada ya muda wa kawaida na kulazimika kuingia kwenye penalti. Gerard Moreno aliwafungia vijana wa Unai Emery kabla ya Edinson Cavani kusawazishia United katika kipindi cha pili. Timu zote zilishindwa kupata ushindi baada ya dakika 30 za nyongeza na kulazimu mechi hiyo kuamuliwa kwa penalti ambapo Villarreal waliibuka washindi.