Katibu Mkuu wa UM atoa wito wa kushikamana na Afrika katika kipindi cha janga la COVID-19
2021-05-27 10:04:44| CRI

 

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kushikamana na Afrika katika mapambano dhidi ya COVID-19 na kurejea kwenye hali ya kawaida baada ya janga.

Akiongea kwenye ufunguzi wa “Mfululizo wa Mijadala ya Afrika 2021”, Bw. Guterres amesema kinachohitajika ni kuelekea kwenye ukuaji endelevu wa uchumi utakaolinda mazingira, kuhimiza haki za binadamu na kuimarisha makubaliano ya kijamii. Amesema ili kufikia Lengo la Maendeleo Endelevu na kutomuacha yeyote nyuma, unahitajika mshikamano imara na ushirikiano wa pande nyingi, pamoja na kuonesha wazi mshikamano na Afrika katika muda huu ambapo bado nchi zinaathirika vibaya na janga la COVID-19.

Akiongea kuhusu chanjo Bw. Guterres amesisitiza kuwa haikubaliki kwamba hadi sasa chanjo haipatikani kwa ukamilifu katika Afrika na kwamba bara hilo lipo nyuma kabisa katika utoaji wa chanjo, lakini amesisitiza kuwa anaamini lazima chanjo iwe nafuu na kupatikana kila mahali.