Wawakilishi wa mazungumzo ya kibiashara ya China na Marekani wafanya mazungumzo kwa simu
2021-05-27 19:10:27| CRI

Naibu waziri mkuu wa China ambaye pia ni kiongozi wa upande wa China katika mazungumzo ya kiuchumi kati ya China na Marekani Bw. Liu He na mwakilishi wa mazungumzo ya kiuchumi wa Marekani Katherine Tai leo wamefanya mazungumzo kwa njia ya simu.

Pande hizo mbili zimefanya mawasiliano ya wazi na kiujenzi, kwa msimamo wa usawa na kuheshimiana, na kukubaliana kuwa ni muhimu kuendeleza biashara kati ya pande hizo mbili. Pia viongozi hao wamebadilishana maoni kuhusu masuala yanayofuatiliwa na kila upande, na kukubaliana kuendelea na mawasiliano.