Watu wanane na mfyatuaji risasi wauawa kwenye shambulizi la San Jose jimboni California Marekani
2021-05-27 10:05:49| CRI

 

 

Watu tisa akiwemo mtu mwenye silaha wameuawa na mmoja kujeruhiwa Jumatano asubuhi kwenye shambulizi la kufyatua risasi katika eneo la Mamlaka ya Usafiri ya Valley (VTA) kaskazini mwa San Jose jimboni California Marekani.

Mkuu wa polisi ya Kaunti ya Santa Clara amethibitisha tukio hilo na kusema watu wanane wamefariki papo hapo kwenye tukio na mmoja kupelekwa hospitali, hata hivyo hakutoa maelezo ya kina juu ya hali yake. Maafisa wa polisi wamemtambua mtu mwenye silaha kuwa ni Samuel Cassidy mwenye umri wa miaka 57 ambaye ni mfanyakazi wa matengenezo, na sababu ya kufanya hivyo bado haijajulikana.