China yaongoza duniani katika maendeleo ya mtandao wa 5G
2021-05-27 10:08:09| CRI

 

 

China imechukua nafasi ya uongozi duniani katika maendeleo ya mtandao wa 5G, na vituo 819,000 vya 5G vimejengwa, idadi ambayo inachukua zaidi ya asilimia 70 ya jumla ya vituo hivyo kote duniani.

Naibu waziri wa viwanda na Tehama wa China Liu Liehong ametangaza takwimu hizo kwenye Maonesho ya Viwanda vya Big Data ya Kimataifa ya China yanayoendelea huko Guiyang, mji mkuu wa mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China.

Kwa mujibu wa ofisa huyo, idadi ya vifaa vilivyounganishwa kwenye mtandao wa 5G nchini China imezidi milioni 310, idadi inayochukua zaidi ya asilimia 80 ya jumla ya dunia nzima.