Majadiliano kuhusu makubaliano ya kitaasisi kati ya Uswisi na Umoja wa Ulaya yamalizika bila kufikia maafikiano
2021-05-27 16:26:47| Cri

Baraza la Jamhuri la nchini Uswisi limetangaza jana kuwa, halitasaini makubaliano ya kitaasisi na Umoja wa Ulaya, hivyo kumaliza majadiliano yaliyodumu kwa miaka saba.

Rais wa Uswisi Guy Parmelin ameutaarifu Umoja huo kuwa, masharti yaliyotakiwa hayakutimizwa, na hivyo kumaliza majadiliano zaidi kuhusu uwezekano wa kufikia makubaliano na Kamati ya Ulaya.

Majadiliano juu ya makubaliano ya kitaasisi yalianza mwaka 2014 ili kuhakikisha Uswisi inaingia kwenye soko moja la Ulaya, na kuwezesha kutatua mfumo wa mgogoro na kudumisha uhusiano mzuri na Umoja wa Ulaya.

Hata hivyo, majadiliano yalisimama tangu mwezi Novemba mwaka 2018 kutokana na pande zote mbili kushindwa kuelewana kuhusu maeneo matatu muhimu ya makubaliano hayo.