China na Uganda zasaini makubaliano ya kutambuana kwenye AEO
2021-05-28 09:44:12| CRI

 

Mamlaka ya Forodha ya China (GACC) imesema, China na Uganda zimesaini makubaliano ya forodha juu ya hadhi ya Msimamizi wa Eneo la Kiuchumi (AEO) hatua ambayo itarahisisha biashara kati ya nchi mbili.

GACC imesema haya ni makubaliano ya kwanza ya kutambuana kwenye AEO ambayo yamesainiwa na China na nchi za Afrika. Chini ya makubaliano, kampuni zilizopata hadhi ya AEO za nchi mbili zitanufaika na taratibu rahisi za forodha, kama vile kupunguza uchunguzi ama kupewa kipaumbele kwenye kupatiwa kibali wakati wanaposafirisha bidhaa kwenye nchi nyingine.

Kwa mujibu wa GACC China imesaini makubaliano ya pande mbili ya AEO na nchi na sehemu 46, na kuwa nchi ya kwanza duniani kwa upande wa idadi kubwa ya makubaliano.