Waziri mkuu wa China kuhudhuria Mkutano wa pili wa mwaka 2030 wa wenzi wa malengo ya kijani duniani
2021-05-28 19:10:11| Cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Zhao Lijian amesema, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang atahudhuria Mkutano wa pili wa wenzi wa malengo ya kijani wa mwaka 2030 kwa njia ya video utakaofanyika Mei 30.

Bw. Zhao amesema, kitendo cha Waziri mkuu wa China kuhudhuria mkutano huo kumeonesha nia ya China ya kushiriki na kuchangia mambo ya usimamizi wa hali ya hewa duniani, na kuhimiza uwajibikaji wa nchi kubwa kwa ufufukaji wa uchumi wa kijani baada ya janga la virusi vya Corona.

Pia amesisitiza kuwa, China inapenda kuendelea kushirikiana na jamii ya kimataifa, kuhimiza usimamizi wa mazingira duniani, kutimiza ufufukaji shirikishi wa kijani duniani, ili kujenga jumuiya ya pamoja ya maisha ya binadamu na mazingira ya kiasili.