Rais wa China apongeza kongamano la nadharia ya vyama vinavyofuata Umarx Duniani
2021-05-28 15:07:50| CRI

Katibu mkuu wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China ambaye pia ni rais wa China Bw. Xi Jinping ametuma barua ya pongezi kwenye kongamano la nadharia ya vyama vinavyofuata Umarx Duniani.

Kwenye barua yake Rais Xi amesema, nadharia ya Umarx inaonesha maendeleo ya jamii ya binadamu, na kudhihirisha njia ya kutafuta ukombozi wa binadamu, kuhimiza maendeleo ya ustaarabu wa binadamu, na ni silaha ya mawazo yenye nguvu inayosaidia kuelewa dunia na kurekebisha dunia.

Rais Xi alisisitiza kuwa, ili kukabiliana na changamoto ya pamoja inayoikabili jamii ya binadamu, vyama vinavyofuata Umarx duniani vinapaswa kuimarisha mawasiliano, chama cha kikomunisti cha China kinapenda kushirikiana na vyama vya nchi mbalimbali vinavyofuata Umarx kuhimiza maendeleo ya jamii ya binadamu na kujenga mustakabli wa pamoja wa binadamu.