Uwekezaji wa China katika nchi za nje waendelea kuongezeka
2021-05-28 09:42:24| CRI

 

 

Takwimu zilizotolewa na Wizara ya Biashara ya China zinaonesha kuwa, katika miezi minne iliyopita, uwekezaji wa moja kwa moja uliotolewa na China kwa nchi za nje ulifikia yuan bilioni 285.1, sawa na takriban dola bilioni 44.7 za kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 3.3 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hiki.

Msemaji wa wizara hiyo Gao Feng amesema kuanzia mwezi Januari hadi Aprili, uwekezaji wa China kwa nchi za nje katika sekta ya uzalishaji ulifikia dola bilioni 5.72, na kuongezeka kwa asilimia 23.5 ikilinganishwa na mwaka jana. Wakati huohuo, uwekezaji wa China kwa nchi za nje pia umeongezeka kwa kasi katika sekta za TEHAMA, utafiti wa sayansi na teknolojia, uchukuzi, afya, huduma za wakazi na nyinginezo.