CMG na serikali ya mkoa wa Hebei zasaini makubaliano ya kuzidisha ushirikiano
2021-05-28 19:52:56| CRI

Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) na serikali ya mkoa wa Hebei leo zimesaini makubaliano ya kuzidisha ushirikiano wa kimkakati, na kuzindua kituo cha CMG mkoani humo.

Hafla ya uzinduzi wa Kituo hicho ilihudhuriwa na Mkuu wa CMG Bw. Shen Haixiong na katibu wa kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China mkoa wa Hebei Bw. Wang Dongfeng .

Bw. Shen amesema, siku zote CMG na serikali ya mkoa wa Hebei zimekuwa na uhusiano na ushirikiano mzuri, na kusaini makubaliano hayo ni hatua yenye nguvu kwa CMG kujifunza kwa kina wazo la ujamaa wenye umaalum wa Kichina katika zama mpya lililotolewa na rais Xi Jinping, na kufungua ukurusa mpya wa ushirikiano wa kimkakati kati ya pande hizo mbili.