China yasisitiza kufufua uchumi wa kijani ili kujenga siku nzuri za baadaye kwa binadamu wote
2021-05-31 08:49:00| Cri

China yasisitiza kufufua uchumi wa kijani ili kujenga siku nzuri za baadaye kwa binadamu wote_fororder_李克强 2

Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amesema China inapenda kushirikiana na pande nyingine kufufua uchumi wa kijani ili kujenga siku nzuri za baadaye kwa binadamu wote.

Bw. Li Keqiang amesema hayo kwa njia ya video kwenye mkutano wa pili wa kilele wa wenzi wa ukuaji wa uchumi wa kijani na malengo ya dunia ifikapo mwaka 2030 ulioitishwa na Korea Kusini. Amesema maendeleo endelevu ya kijani ya dunia yanakabiliwa na changamoto kubwa wakati uchumi wa dunia unakosa utulivu kufuatia sintofahamu nyingi zinazosababishwa na janga la virusi vya Corona.

Bw. Li pia amesema pande mbalimbali za jamii ya kimataifa zinatakiwa kusaidiana na kushirikiana ili kuhakikisha maendeleo na mageuzi ya uchumi wa kijani yanakwenda sambamba, kusaidiana na kuboresha sifa ya maendeleo. Ameongeza kuwa ikiwa nchi kubwa inayoendelea, China inafanya juhudi kubwa ili kutimiza lengo la kujijenga kuwa nchi ya kisasa ifikapo katikati ya karne hii huku ikitafuta maendeleo yasiyotoa kaboni nyingi.