Mkuu wa UM atoa wito wa kuwepo kwa ushirikiano wa kimataifa kutafuta ukuaji wa uchumi wa kijani
2021-05-31 08:49:25| Cri

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa wito wa kuwepo kwa ushirikiano wa kimataifa ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutafuta ukuaji wa uchumi shirikishi wa kijani.

Bw. Guterres amesema hayo kwa njia ya video kwenye mkutano wa pili wa kilele wa wenzi wa ukuaji wa uchumi wa kijani na malengo ya dunia ifikapo mwaka 2030 ulioitishwa na Korea Kusini. Ameuambia mkutano huo kuwa kauli mbiu ya pendekezo hilo imeeleza vya kutosha kitu kinachohitajika duniani kwa sasa ni ushirikiano wa kimataifa: yaani kushirikiana kupambana na virusi vya Corona na kujenga ufufuaji mzuri, kushirikiana kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu na kushirikiana kushughulikia mabadiliko ya tabia nchi.