Kitendo cha Marekani kuzuia ushirikiano wa kupambana na janga la COVID-19 duniani kinaonesha uovu
2021-06-01 09:12:14| Cri

Wakati wa mkutano wa 74 wa Baraza la Afya Duniani (WHA) uliofanyika kuanzia Mei 24 na kumalizika leo Juni, jamii ya kimataifa kwa ujumla ilikuwa na matarajio ya kuimarisha ushirikiano wa kupambana na janga la COVID-19 duniani ili kuvitokomeza virusi na kurejesha ukuaji wa uchumi mapema zaidi.

Hata hivyo baadhi ya wanasiasa na vyombo vya habari vya Marekani wamerejesha tena dhana ya kwamba virusi vya COVID-19 vimetoka kwenye maabara ya China, jambo ambalo limethibitishwa na utafiti wa kisayansi kuwa si kweli, na kujaribu kutunga nadharia mpya ya njama kuhusu chanzo cha virusi na kuleta ujanja wa kisiasa wa kuikashifu na kuisingizia China kuwa ndio imesababisha mlipuko.

Vitendo hivyo viovu vya Marekani vinaonesha kwamba hawaiheshimu sayansi na wala hawabebi wajibu juu ya maisha ya watu, na hakika vitavunja ushirikiano wa kupambana na janga duniani.

Kufuatilia virusi ni suala la kisayansi ambalo ni tata na ni kubwa sana, na suluhu inapaswa kufikiwa kwa misingi ya kisayansi.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa Machi 30 na Shirika la Afya Duniani (WHO) juu ya utafiti uliofanywa kwa pamoja na China na WHO kuhusu chanzo cha COVID-19, virusi vya Corona “haviwezekani kabisa” kutoka kwenye maabara. Utafiti huo wa pamoja, uliofanywa na wataalamu wa China na nchi za kigeni, ulifikia makubaliano sawa chini ya msingi wa utafiti wa kisayansi na ukweli, ikimaanisha kuwa matokeo ya utafiti ni ya kweli, ya kisayansi, na ya kuaminika. Wataalamu wa kigeni waliojiunga kwenye utafiti, wote walichaguliwa na WHO, ambao wametoka nchi 10 pamoja na WHO yenyewe.

China kila mara inakuwa mkweli na mdhati katika kufuatilia chanzo cha virusi, na kuweka mfano wa kuhimiza ushirikiano wa kimataifa katika kutafuta chanzo cha COVID-19. Ingawa ilikabiliwa na kazi ngumu ya kudhibiti janga nyumbani, China iliwaalika wataalamu wa WHO kufanya utafiti wa chanzo cha COVID-19 na kutoa usaidizi wa kutosha kwenye kazi yao huko Wuhan, mji ambao ni kitovu cha virusi nchini, na kuonesha uwazi na mtazamo wa uwajibikaji.

Wataalamu wengi wa kigeni walisema kwamba uwazi wa China haukutarajiwa, na safari ya Wuhan ilionesha matokeo ya kushangaza. Ushahidi, ripoti na tafiti nyingi zinaonesha kwamba janga lilionekana kwenye maeneo mengi duniani mwanzoni mwa nusu ya pili ya mwaka 2019. Iliripotiwa kuwa virusi vilianza kushambulia Marekani mapema zaidi kuliko nchi iliyoripoti rasmi mgonjwa wa kwanza aliyethibitishwa.

Wakati Marekani ikiitaka China kushiriki kwenye uchunguzi wa kimataifa ambao ni wa kina, uwazi, na ulio chini ya msingi wa ushahidi, na yenyewe pia inapaswa kufanya hivyohivyo. Inatakiwa kuwa na mtazamo wa kisayansi, kushirikiana na WHO mara moja kwenye utafiti wa chanzo cha virusi, kufanya utafiti wa kina, uwazi, na ulio chini ya msingi wa ushahidi nyumbani, na kujibu haraka wasiwasi wa jamii ya kimataifa.

Baadhi ya wanasiasa wa Marekani na vyombo vya habari vimepuuza kabisa ukweli na sayansi, na kutojali mashaka hayo wakati wanafuatilia virusi pamoja na kushindwa kwao sana kwenye mapambano dhidi ya janga nyumbani. Badala yake, wamekuwa wakijihusisha katika kuanzisha na kueneza uwongo, na hata kuamuru bila aibu mashirika ya kiintelijensia kuchimba kuhusu chanzo cha virusi.

Huo ni ushahidi kwamba Marekani haijali ukweli na haina nia ya kufuatilia virusi kwa njia ya kisayansi. Ila wanachotaka ni kunyanyapaa nchi nyingine na kuchezea watu kisiasa kwa kisingizio cha janga. Shutuma za Marekani kwamba maabara ya China ndio imevujisha virusi zinaungwa mkono na “ushahidi kamili” kama walioutoa wakati ilivyokuwa inaishutumu Iraq.

Lakini shutuma za Marekani zimekuwa zikipingwa na WHO na jamii ya kimataifa ya wanasayansi. Mei 28, WHO kwa mara nyingine tena ilitaka suala la uchunguzi wa chanzo cha virusi kutofanywa la kisiasa ili wanasayansi waweze kushughulikia utafiti na kutoa ushahidi unaoaminika. La sivyo, dunia hataitapata majibu sahihi kuhusu chanzo cha virusi.

Kwenye jambo kubwa kama hilo, linalohusiana na usalama wa afya ya umma duniani na maisha ya watu, Marekani imechagua siasa kuliko sayansi kwa maslahi yao binafsi. Vitendo vyake vya kudharauliwa kamwe havitakubaliwa na jamii ya kimataifa.