Mawaziri wa NATO wakubali kuendelea kuiunga mkono Afghanistan baada ya kuondolewa wanajeshi
2021-06-02 09:24:38| Cri

Katibu mkuu wa Shirika la Kujihami la Mataifa ya Magharibi (NATO) Bw. Jens Stoltenberg amesema mawaziri wa mambo ya nje na ulinzi wa shirika hilo jana walikubali kuendelea kuiunga mkono jamii ya Afghanistan baada ya kuondoa vikosi huko Kabul.

Akizungumza na wanahabari Stoltenberg amesema mawaziri hao wameona kuwa hatua hiyo ni njia mwafaka ya kuunga mkono amani ya Afghanistan. Shirika la NATO litaendelea kutuma wanadiplomasia nchini humo baada ya kuondoa vikosi vyake, na kuendelea kuvipatia fedha vikosi vya usalama vya Afghanistan na kuzijengea uwezo taasisi za usalama nchini humo.

Nchi washirika za NATO ziliamua kuanza kuondoa vikosi vyake nchini Afghanistan kabla ya tarehe mosi mwezi Mei, na kupanga kumaliza kuondoa vikosi ndani ya miezi michache.