China yataka kuwepo kwa ushirikiano wa BRICS
2021-06-02 09:21:14| Cri

Mjumbe wa Baraza la Taifa la China na Waziri wa Mambo ya Nje Bw. Wang Yi ametoa wito kwa nchi za BRICS kuhimiza mshikamano kote duniani, kushughulikia matatizo yaliyojitokeza katika utatuzi wa masuala ya kimataifa na kukabiliana na changamoto za pamoja.

Kwenye mkutano uliofanyika kwa njia ya video na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za BRICS yaani Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini, Wang amezitaka nchi hizo kuimarisha mshikamano wa kimataifa katika kupambana na janga la virusi vya Corona na kuwa walinzi wa afya ya watu.

Akielezea kuwa China imetoa zaidi ya dozi milioni 350 za chanjo ya COVID-19 kwa jamii ya kimataifa, Wang alisema inatarajiwa kuwa BRICS itaendelea kufanya chanjo kuwa bidhaa ya umma duniani, kushikilia kanuni ya usambazaji wenye haki na usahihi, kuunga mkono Shirika la Afya Duniani kuongeza kasi ya kutekeleza mpango wa COVAX na kuunga mkono Shirika la Biashara Duniani kufanya maamuzi mapema kuhusu kusamehe hakimiliki za ujuzi za chanjo hiyo.