Naibu waziri mkuu wa China na waziri wa fedha wa Marekani wazungumza kwa video
2021-06-02 11:06:44| Cri

Naibu waziri mkuu wa China Liu He amezungumza kwa njia ya video na waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen.

Pande hizo mbili zinaamini kuwa uhusiano wa kiuchumi kati ya China na Marekani ni muhimu sana. Zikifuata msimamo wa usawa na kuheshimiana, zimefanya mawasiliano kwa kina juu ya hali ya jumla ya uchumi, na ushirikiano wa pande nyingi na pande mbili, kubadilishana maoni kwa moyo wa dhati juu ya masuala zinazoyafuatilia kwa pamoja, na wako tayari kuendelea kudumisha mawasiliano.