Huawei na chuo kikuu cha Ethiopia zazindua kituo cha mafunzo ya TEHAMA
2021-06-02 09:20:55| Cri

Kampuni ya teknolojia ya China Huawei na Chuo Kikuu cha Addis Ababa, Ethiopia zimezindua Kituo cha Mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika taasisi ya teknolojia ya chuo kikuu hicho mjini humo.

Kituo hicho kitatoa mafunzo ya kiutendaji na uzoefu wa uvumbuzi kwa wanafunzi na wataalam wa sekta hiyo, ikiwa na lengo la kuandaa wahandisi zaidi ya elfu 2 wakiwemo wanafunzi na walimu ili kuboresha utaratibu wa uandaaji wataalam nchini Ethiopia katika miaka mitatu ijayo. Mpango huo umewekezwa kwa kiasi cha dola za kimarekani milioni 2.1, ukiwemo ufadhili wa vifaa vyenye thamani ya dola milioni 1.9.