Kiongozi wa upinzani wa Israel asema wamefikia makubaliano ya kuunda serikali ya awamu mpya
2021-06-03 09:03:24| CRI

Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Israel Yair Lapid amesema kuwa wamefikia makubaliano ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa, ambayo itamaliza utawala wa miaka 12 wa waziri mkuu Benjamin Netanyahu.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Lapid kutoka mrengo wa kati na mwenzi wake mkuu Naftali Bennett imetolewa dakika 30 kabla ya muda wa mwisho wa kuunda serikali mpya ya umoja kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 23, Machi.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais Reuven Rivlin wa Israel imesema Lapid amemwarifu rais kuwa ameweza kuunda serikali moja.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Lapid, kiongozi wa chama cha mrengo wa kati cha Yesh Atid na Naftali Bennett, kiongozi wa chama cha wazalendo Yamina watashika wadhifa wa uwaziri mkuu kwa zamu, ambapo Bennett atashika zamu kwanza kwa miaka miwili.