Mjumbe wa China:Masuala halali ya Iran yapaswa kushughulikiwa ipasavyo
2021-06-03 09:27:35| cri

Mjumbe wa China amesema kwamba masuala halali ya Iran yanapaswa kushughulikiwa ipasavyo katika mazungumzo yanayoendelea ya kufufua makubaliano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015, yanayojulikana rasmi kama Mpango wa Utekelezaji wa Pamoja (JCPOA).

Mjumbe wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Wang Qun na mashirika mengine ya kimataifa huko Vienna amesema hayo baada ya mkutano wa hivi karibuni wa Tume ya Pamoja ya JCPOA.

Mjumbe huyo amesisitiza kuwa China daima inashikilia msimamo usio na upendeleo juu ya suala la nyuklia la Iran na iko tayari kuendelea kufanya kazi na pande zote zinazohusika kusukuma mbele mazungumzo hayo. Aliongeza kuwa China pia itaendelea kulinda haki na maslahi yake halali katika kuondoa vikwazo na mambo mengine.