WHO kuidhinisha chanjo ya Sinovac ya China kwa matumizi ya dharura kunaonesha usalama na ufanisi wa chanjo ya China
2021-06-03 08:33:55| Cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema baada ya kukaguliwa na kupitishwa kwa chanjo ya COVID-19 iliyotengenezwa na Kampuni ya China ya Sinopharm, chanjo nyingine ya China ya Kampuni ya Sinovac imeidhinishwa tena, hali ambayo imeonesha vya kutosha usalama na ufanisi wa chanjo na ufundi unaohusika wa China, na kutoa vifaa vingi zaidi kwa ajili ya kushinda mapema katika mapambano dhidi ya virusi.

Bw. Wang ameeleza kuwa, China itaendelea kuunga mkono makampuni ya chanjo ya China kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na Shirika la Afya Duniani WHO na mipango ya utekelezaji kuhusu virusi vya Corona, kuyahamasisha makampuni mengi zaidi ya China kufanya ushirikiano kwenye utafiti na wenzi nje ya nchi, uendelezaji na uzalishaji, ili kuzisaidia nchi nyingi zinazoendelea duniani kupata chanjo.

Siku hiyo hiyo rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amekaribisha hatua ya WHO ya kutoa idhini ya matumizi ya dharura ya chanjo ya COVID-19 ya Kampuni ya Sinovac ya China. Akisema kipaumbele ni kuielekeza Idara ya usimamizi wa bidhaa za afya ya nchi hiyo Sahpra kufikiria namna ya kuingiza chanjo ya Sinovac.