Xi ampa pole mwenzake wa Namibia
2021-06-04 09:05:13| Cri

Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za pole kwa mwenzake wa Namibia Hage Geingob baada ya yeye na mkewe kuambukizwa virusi vya Corona, na kuwatakia wapone haraka.

Kwenye salamu zake, rais Xi pia alisema tangu kuibuka kwa janga la virusi vya Corona, China na Namibia zimeungana mkono na kupambana na ugonjwa huo bega kwa bega, na urafiki wao wa jadi umeimarishwa zaidi.

Rais Xi amesema anatilia mkazo sana umuhimu wa kukuza uhusiano kati ya China na Namibia, na kuwa tayari kufanya kazi na rais Geingob ili kuinua uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili kwenye kiwango kipya.