Mkuu wa kupambana na ufisadi wa China ataka kuwepo ushirikiano wa kimataifa dhidi ya ufisadi
2021-06-04 10:44:43| Cri

Afisa wa ngazi ya juu wa China anayeshughulikia kupambana na ufisadi amezitaka pande zote kuungana pamoja na kufuata mtazamo wa jamii ya binadamu yenye hatma ya pamoja na kujenga dunia isiyo na ufisadi.

Zhao Leji, katibu wa kamati kuu inayoshughulikia Ukaguzi wa Nidhamu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC, amesema hayo kwenye mkutano maalumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya changamoto na hatua za kuzuia na kupambana na ufisadi na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa.

Bw. Zhao amesema China inaipongeza UM kwa juhudi na mchango wake katika kuzuia na kupambana na ufisadi, na inaunga mkono kwa dhati Mkataba wa UM wa kupambana na Ufisadi (UNCAC) unaotumika kama njia kuu ya utawala wa kupambana na ufisadi. Amesema CPC na serikali ya China ina msimamo sawa dhidi ya ufisadi, na imeendelea kuboresha mfumo wa uangalizi wa kisoshalisti wenye umaalumu wa kichina na CPC kutumia njia zenye ufanisi kujisafisha kama chama tawala cha muda mrefu.