China, Afghanistan na Pakistan zafikia makubaliano ya kuhimiza mchakato wa amani na kupamba na ugaidi nchini Afghanistan
2021-06-04 09:14:26| Cri

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Wang Yi jana aliendesha Mazunguzo ya 4 kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za China, Afghanistan na Pakistan mjini Guiyang, China, ambapo waziri wa mambo ya nje wa Afghanistan Bw. Mohammad Haneef Atmar na mwenzake wa Pakistan Bw. Shah Mahmood Qureshi wamehudhuria mazungumzo hayo.

Wang Yi amesema hali ya sasa yenye utatanishi ya kimataifa na kikanda inabadilika sana, hali ambayo inailetea Afghanistan changamoto mpya kwa usalama na utulivu wake. Uondoaji vikosi vya nchi za nje nchini Afghanistan unauathiri mchakato wa amani nchini humo, na mapambano na shughuli za kigaidi zimetokea mara kwa mara. Kutokana na hali hiyo, nchi hizo tatu zinapaswa kuimarisha mawasiliano na ushirikiano, ili kulinda maslahi ya Afghanistan na nchi nyingine zilizoko kwenye kanda hiyo.

Mawaziri hao wa nchi tatu wamefikia makubaliano juu ya mchakato wa amani na mapambano dhidi ya ugaidi nchini Afghanistan, pamoja na ushirikiano kati ya nchi hizo tatu.