China yaitaka Marekani kukomesha kitendo chake cha kupeleleza watu kisiri
2021-06-04 08:52:51| Cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China Wang Wenbin ameitaka Marekani kukomesha kitendo chake cha kupeleleza kisiri na kuilipa dunia kwa deni lake la kutoitendea haki.

Akijibu shutuma za hivi karibuni zilizotolewa na viongozi na maafisa wa Ulaya kuhusu Shirika la Usalama wa Taifa la Marekani kuwachunguza kisiri viongozi wa washirika wake, Bw. Wang amesema kama washirika wa Marekani wanaona tabia ya kuwachunguza haikubaliki, basi dunia ndio inaona haikubali zaidi.

Bw. Wang amesema Marekani inajulikana zamani duniani kuwa ni bingwa wa kuiba siri, na kusema njia inazotumia ni pamoja na kuiba data kwenye simu za mkononi, kugeuza app za simu za mkononi kama kifaa cha uchunguzi, kuingia kwenye seva ya mawingu, kunasa mikonga ya simu chini ya bahari, kuweka vituo vinavyokusanya ishara za uchunguzi kisiri kwenye karibu balozi na konseli kuu 100 duniani kwa lengo la kufanya upelelezi. Hivyo ameitaka Marekani kuacha biashara chafu ya kuwakandamiza washirika wake wengine kwa kisingizio cha usalama wa taifa.