Mjumbe wa kudumu wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya CPC Zhao Leji ahudhuria mkutano maalumu wa UM wa mapambano dhidi ya ufisadi
2021-06-04 11:37:07| cri

Mjumbe wa kudumu wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisiti cha China CPC ambaye pia ni katibu mkuu wa kamati ya nidhamu ya chama Bw. Zhao Leji amehudhuria na kuhutubia mkutano maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mapambano dhidi ya ufisadi kwa njia ya video.

Bw. Zhao amesema Chama cha Kikomunisiti cha China na serikali ya China inapambana kithabiti na ufisadi, huku ikiendelea kuboresha mfumo wa usimamizi wa ujamaa wenye umaalum wa China, kuchunguza na kutafuta njia ya kujisafisha katika hali ya utawala wa muda mrefu. Rais Xi Jinping wa China pia anatilia maanani mapambano dhidi ya ufisadi, kamati kuu ya chama inatoa uongozo wa pamoja kwa mapambano dhidi ya ufisadi, ili kutoa mwongozo na uhakikisho wenye nguvu zaidi katika mapambano hayo.

Bw. Zhao pia ametoa mapendekezo manne kuhusu ushirikiano wa kimataifa katika mapambano dhidi ya ufisadi, ambayo ni pamoja na kuwa na msimamo wa kutovumilia ufisadi, kujenga mfumo usio na ufisadi na kuanzisha ushirikiano kwenye mapambano dhidi ya ufisadi usio na kizuizi, kuheshimu haki ya nchi mbalimbali kuchagua njia tofauti za kupambana na ufisadi, na kuboresha utaratibu wa kimataifa wa kupambana na ufisadi.